LONDON, England
MSHAMBULIAJI, Cristiano Ronaldo, ameiambia Manchester United kuwa wanahitaji kushinda taji la Ligi Kuu ya England.

Hiyo ni baada ya kurejea klabuni hapo baada ya miaka takribani 12.Nyota huyo amerejea Old Trafford wakiwa tayari wameshakusanya pointi saba kati ya tisa kwenye Ligi Kuu ya England mismu huu, kwa sasa wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Kwa mujibu wa gazeti la ‘The Sun’, mshindi huyo wa mara tano wa ‘Ballon d’or’ amewaambia wanatimu wenzake kuwa ana hamu kubwa ya kupata ushindi huo sasa, na ni wakati wa klabu hiyo kushinda.Chanzo kutoka ndani ya klabu kimeripoti kuwa wachezaji wamefurahi kumpokea Ronaldo na wameona wamepata morali na ujasiri zaidi.

Chanzo kinasema, wachezaji na makocha kwa sasa wanaamini wana kikosi bora kwenye ligi na wanaweza kutwaa taji.Chanzo hiki kimenukuliwa kikisema: “Ronaldo amezungumza na Bruno Fernandes, akimwambia kuwa timu inahitaji kushinda EPL kwa sasa”. (Goal).