LONDON, England
CHELSEA inakutana na kikwazo katika jitihada za kumshawishi nyota wake, Antonio Rudiger kusaini mkataba mpya Stamford Bridge.
Beki huyo wa kati mwenye uraia wa Ujerumani ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu chini ya Thomas Tuchel, tayari ameingia kwenye miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja huko England, ofa ya hivi karibuni ya Chelsea ya mkataba mpya wa Rudiger ilikweenda tofauti huku marekebisha zaidi yakishauriwa kufanyika kwenye mkataba huo.
Mkataba wa nyota huyu mwenye miaka 28 unafuatiliwa na klabu kadhaa kubwa ikiwemo Real Madrid, Bayern Munich, Paris Saint-Germain, Juventus na Atletico Madrid.
Lakini, Tottenham Hotspurs ndiyo wanaotajwa kuwa wapinzani pekee wa EPL wanaojaribu kuonesha nia ya kumtaka nyota huyo. Awali Spurs walishajaribu kuinasa saini yake.
Wakati sekeseke la mkataba mpya wa Rudiger zikiendelea, mpaka sasa beki huyo amecheza zaidi ya mechi 150 na Chelsea tangu alipowasili klabuni hapo mwaka 2017.
Wakati huo huo, mshambuliaji, Antoine Griezmann, amesema,
alitaka kurejea Atletico Madrid kutokana na namna aliyokuwa klabuni hapo awali.
Griezmann aliifungia Ufaransa magoli mawili dhidi ya Finland katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwaka 2022 na kumaliza ukame kwa timu ya Didier Deschamps, kutoshinda mechi mbili.
Mara baada ya mchezo huo, Griezmann alifuguka akiwa kama mchezaji wa Atletico Madrid kwa awamu ya pili aliweka wazi kwamba anatarajia kuweka uhusiano mzuri na mashabiki wa klabu.Ikiwa hiyo itafanyika mara moja haijulikani, hasa baada ya machafuko ambayo yalitokana na jinsi Griezmann alivyoondoka kwenda Barcelona.“Nadhani kumekuwa na uhusiano mzuri kati ya mashabiki na mimi, nataka kuupata tena’.