NA VICTORIA GODFREY

KAMATI ya maandalizi ya  Tamasha la Michezo la Wanawake lililopewa jina la ‘Tanzanite women  sports Festival 2021’ imethibitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuzindua tamasha hilo ambalo  limepangwa kufanyika kuanzia Septemba 16 – 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa na Uhuru.

Mwenyekiti wa Kamati  hiyo Neema Msitha,alisema  maandalizi yameendelea kupamba moto na tayari klabu za michezo mbalimbali zimethibitisha ushiriki wao na zinaendelea na mazoezi.

Alisema klabu shiriki ni zile zilizoshika nafasi ya kwanza na ya pili katika ligi zao ili kuleta ushindani na hamasa ya kuenzi na kuthamini michango wa wanawake waliofanya vizuri katika tasnia ya michezo.

” Uwepo wa mpango huu umekuja baada ya kuona wapo wanawake walifanya vizuri kitaifa na kimataifa lakini hawaenziwi,hivyo hii ni fursa ya kuwatambulisha kutokana na bado kundi hili tuko nyuma katika michezo  na tuna nafasi kubwa ya ushindi tunataka kuhamasisha ushiriki kupitia tukio hili,” alisema Neema.

Michezo itakayoshindaniwa ni  netiboli JKT Mbweni watavaana dhidi ya Uhamiaji,huku Kikapu JKT watamenyana dhidi ya BD Lioness, na watu wenye Ulemavu wakati Soka Simba watatupa karata yake dhidi ya U-20.

Michezo mingine Wavu Jeshi Star watapambana  dhidi ya Magereza, michezo ya jadi ikiwamo nage,kuvuta kamba,kukuna nazi, kuruka kamba na  ngumi za kulipwa na riadha