WASHINGTON, MAREKANI

WAZIRI wa fedha wa Marekani Janet Yellen ametahadharisha kwamba serikali ya Marekani inaweza kuishiwa fedha mwezi ujao na amelitaka bunge la nchi hiyo liongeze uwezo wa serikali wa kukopa.

Waziri Yellen alitoa tahadahri hiyo katika barua aliyomwandikia spika wa bunge Nancy Pelosi.

Katika barua hiyo Waziri huyo alisema ikiwa bunge halitaongeza kima cha mikopo, serikali ya Marekani itaishiwa fedha mwezi ujao wa Oktoba na kwamba kwa mara ya kwanza katika historia yake Marekani haitokuwa na uwezo wa kutimiza dhima zake za kifedha.

Deni la serikali ya Marekani liliongezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa janga la COVID-19 baada ya serikali hiyo kupitisha mipango mitatu ya matumizi makubwa ili kupunguza athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga hilo.