NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Simba unatarajia kuzindua jezi zao mpya za msimu wa 2021/22 Jumamosi hii.Hayo yamezungumzwa jana kwenye mkutano wa Simba na watengenezaji wa jezi hizo Vunjabei uliofanyika hoteli ya Kilimanjaro Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Vunja Bei Fred Ngajiro alisema uzinduzi wa jezi hizo utafanyika Septemba 4, saa 1:00 usiku.

“Uzinduzi wetu wa jezi tutaizundua Septemba 4, saa 1:00 usiku na jezi yetu itakuwa nzuri sana kushinda jezi za timu nyingine hizi za ndani.Alisema jezi hizo zitapatikana rasmi kwenye maduka yote ya Vunjabei mara baada ya kuzinduliwa.

“Kuna jezi nyingi ambazo zimesambaa watu wanatangaza ndio jezi za Simba sio kweli, sisi jezi zetu bado hazijasambaa na zitakuwa jezi namba moja kuwahi kutokea,” alisema

Kwa upande mwingine msanii Whozu ambaye aliambatana na Vunjabei alisema kwamba ameachia wimbo rasmi wa Simba ambao utakuwa unaitwa Simba ni Noma ambao amemshirikisha msanii Donat Mwanza kutoka nchini Congo.