NA ALI MAHFOUDH, ABUBAKAR SHOMARI, (TUDARCo)

WAZIRI wa Afya, Wanawake, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui, amesema Wizara yake itashirikiana na Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA), ili kuzalisha wahudumu bora wa Afya hasa wa fani ya Physiotherapia.

Waziri huyo aliyasema hayo katika maadhimisho ya kumi na Saba  siku ya madaktari wa Physiotherapia kitaifa yaliyoandaliwa na kada ya afya katika chuo Kikuu Cha Taifa SUZA,  yaliyofanyika katika ukumbi wa taasisi hiyo, Mjini Zanzibar

Amesema amejifunza umuhimu wa Physiotherapia na nafasi yake katika kupambana na ugonjwa wa Uviko-19, hivyo serikali itahakikisha kuzitatua changamoto inazozikabili kada hiyo ikiwemo ya uhaba wa walimu pamoja na vifaa vya kujifundishia

Alisema hatua hiyo itasaidia wanafunzi wafanye mazoezi kwa vitendo na kuwawezesha kupata uzoefu wa kazi zao wakati wakiwa chuoni.