MOGADISHU, SOMALIA
RAIS wa Somalia Maxamed Cabdulaahi Maxamed amesema,urafiki kati ya watu wa Somalia na China una historia ndefu, na China ni mwenzi thabiti wa Somalia.
Katika hafla ya kupokea hati ya utambulisho ya balozi mpya wa China nchini Somalia,Fei Shengchao rais Maxamed alisema katika miaka ya hivi karibuni,uhusiano wa nchi hizo mbili umeimarishwa na ushirikiano wa kimataifa umeongezeka zaidi.
Alisema Somalia inatarajia kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na China na kukuza maendeleo makubwa ya ushirikiano kati yao.
Kwa upande wake, Balozi Fei alisema, China inazingatia maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili na kupongeza ukarabati wa amani nchini humo kuendelezwa kwa madhubuti.
Alisema tangu mripuko wa janga la COVID-19 utokee,China na Somalia zimeshirikiana kupambana na janga hilo na kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano,urafiki na mshikamano.