KHARTOUM, SUDAN

MAOFISA nchini Sudan wanachunguza shehena ya silaha iliyowasili nchini humo kutoka Ethiopia kwa njia ya ndege.

Maofisa hao wanashuku kwamba makasha hayo 72 ya silaha yalikusudiwa kutumiwa kufanya uhaini au uhalifu dhidi ya taifa hilo.

Hayo ni kulingana na ripoti ya kwenye shirika la Habari linalomilikiwa na serikali nchini humo SUNA.

Kamati inayochunguza silaha hizo ilibaini kwamba ziliwasili nchini Ethiopia zikitoka Moscow Urusi mnamo Mei 2019.

Lengo halisi la silaha hizo halijabainika,lakini kamati hiyo inakisia zilikusudiwa kutumiwa na waliokuwa watiifu wa serikali ya zamani ya Bashir,kuhujumu mchakato wa mpito.