KILA mamlaka ama utawala hasa wenye nguvu mara nyingi kunakuwa na mtu muhimu nyuma ya pazia anayetekeleza majukumu nyeti kuifanya mamlaka hiyo kusalia na nguvu zake.

Sina shaka wengi wetu hatulifahamu ama tunalifahamu kidogo sana jina la Vladislav Surkov, ambaye ni mwanasiasa mwenye nguvu na ushawishi mkubwa nyuma ya utawala wa rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Vladislav Surkov ni mwanasiasa na mfanyabishara mashuhuri nchini Urusi, ambaye amezaliwa Septemba 21 mwaka 1964, ambapo kwa miaka 19 amekuwa kama moyo wa serikali ya Urusi, huku akipachikwa majina mengi.

Kuna wakati aliitwa kadinali wa kijivu ‘grey cardinal’ wa ikulu ama serikali ya Urusi akitambulika pia kama mchoraji ama mwandishi wa mifumo ya kisiasa ya rais Vladmir Putin.

Surkov ndiye muanzilishi wa dhana ya demokrasia huru na ndiye jicho la vyombo vya habari vinavyounga mkono propaganda za Putin na kuna wakati alitajwa kama mtu wa pili kwa ushawishi mkubwa nchini Urusi.

Surkov ni miongoni mwa watu wanaonekana kuwa watata nchini Urusi kwa sifa zao na kutoeleweka kwao, lakini ni muhimu kwa uwezo wao na nafasi yake kwenye serikali ya nchi hiyo.

Makala haya yanakuletea mambo sita unayopaswa kujua kuhusu Surkov anayetajwa kama mtu mwenye nguvu zaidi na muhimu asiyefahamika sana ulimwenguni.

Inaaminika Surkov ni miongoni mwa mafundi wakubwa nchini Urusi wa kutengeneza propaganda na misimamo ya nchi Urusi.

Muda mrefu kabla ya rais wa wakati huo, Donald Trump kutumia nguvu kuzima taarifa alizozisema ni ‘potofu’, Surkov alikuwa ndiye anayedaiwa kuzisanifu habari hizo ziliokuwa zikimuudhi Trump.

Zipo taarifa kwamba Surkov ndiye anayetenengeneza mbinu za kuongeza mizozo ya kisiasa kwenye demokrasia huko ulaya ya magharibi.

Surkov ni mtu amenza katika hatua ya kutojulikana mpaka kuwa mtu mwenye nguvu nyuma ya utawala wa Putin nchini Urusi

Surkov ndiye aliyeanzisha ‘Soverign Democracy’, mfumo ambao uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo ulikuwa na matokeo moja tu kuendelea kwa utawala wa Putin.

Mmoja wa watu waliowahi kufanya naye kazi anamuelezea Surkov:’Anadhibiti miundo mbinu na mifumo mingi ya siasa, mifumo hii ni ya utata ni yeye tu Surkov alikuwa anajua inakwendaje”, alisema.

Surkov pia anadaiwa kuwa ndiye kiongozi wa anayesimamia shughuli nyingi ikiwemo mwenendo wa vyama vya siasa, wabunge, magavana, kuanzishwa ama kufungwa na shughuli za kisiasa au mashirika yasiyo kisiasa, makanisa, vyombo vya habari na asasi za kiraia.

Surkov alianzia majukumu yake kama mlinzi. Mikhail Khodorkocsky, aliyehi kuwa miongoni mwa watu matajiri Urusi, alimuajiri Surkov kuwa sehemu ya walinzi wake.

Muda mfupi baadaye mfanyabiashara huyo tajiri alibaini kuwa Sarkov ama mlinzi wake huyo alikuwa na kitu cha ziada kutokana na kuwa na akili na maarifa mengine.

Akaamua kumuhamishia kwenye kitengo chake cha mahusiano (PR) alipoanza kujenga ujuzi wake katika sanaa ya kupika uongo katika mikutano ya kibiashara na kisiasa ya mfanyabishara huyo.

Baada ya kutofautiana, Khodorkovisky akijikuta akiishia kupigwa kifungo jela, ambapo Surkov akilidaiwa alisaidia kuendesha kampeni dhidi ya bosi wake huyo.

Surkov amesomea masuala ya usimamizi wa kumbi za maonyesho jijini Moscow kabla ya kufukuzwa kwa sababu ya kupigana. Ujuzi alioupata ukamsaidia baadae, alipokuwa anasimamia sherehea za ikulu na upinzani. Mmoja wa washauri wa ikulu alisema.

“Alikuwa anajifikiria yeye na kujiona kama mtu anayeendesha shughuli zote, akijaribu kutafuta nafasi kwa kila muigizaji katika kile anachokifanya’, alisema.

Anaongoza vikundi vinavyotaka kujitenga huko Ukraine, nyaraka zilizowah kuvuja kutoka ikulu zinaonyesha kuwa Surkov anaendesha mtandao wa wanahaakati huko mashariki mwa mkoa wa Donbas, ambapo wapiganaji wanaotaka kujitenga wanapambana na serikali ya Kiev itapata msaada kutoka Moscow. Mmoja wa viongozi wa waasi alisema;

‘Mara kwa mara nilikuwa nakutana na Vladislav Surkov. Ni mmoja kati ya watu wenye akili sana niliowahi kukutana nao katika maisha yangu. Kuna wakati nilikuwa namuona kama muigizaji, aliye pekee yake jukwaani. Nimekuwa nikifuatilia maonyesho yake na wakati huo huo najifunza kitu kutoka kwake; Sanaa ya siasa; Sanaa ya hakuna kinachoshindikana’.

Anamzimia Tupac Shakur na Ushauri: ukiingia katika ofisi yake Ikulu alikuwa na picha ya rapa wa Marekani aliyeuawa Tupac Shakur pamoja na picha ya Vladmir Putin. Lakini yeye pia ni mtaalam akimsaidia msanii Jackson Pollock.

Wakati akiendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwenye siasa za Urusi, uliochanganyika na ujanja wa kisanii na siasa za ukatili, amekuwa akipata wasaa wa kuwaandika mashairi wasanii wa bendi ya Agatha Christie inayopiga muziki wa rock nchini Urusi.