NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, kinatarajia kushuka dimbani leo kuvaana na DR Congo.Mchezo huo wakuwania kufuzu kucheza kombe la Dunia utapigwa katika uwanja wa TP Mazembe. Lubumbashi nchini Congo.

Kikosi hicho kimeondoka juzi jioni kuelekea nchini huko kwa ajili ya mchezo huo kikiwa chini ya kocha Kim Paulsen.

Akizungumza kabla yakuondoka nchini kocha Paulsen, aliwataka watanzania kuiunga mkono timu yao na kuwaahidi matokeo mazuri.

“Tunakwenda Congo kushindana kikubwa mashabiki watuombee, kikosi kiweze kufanya vizuri,” alisema

Mara baada ya mchezo huo Taifa Stars watarudi kujiandaa na mchezo dhidi ya Madagascar utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa Tanzania.