NA MWADISHI WETU

TIMU ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na kocha mkuu, Kim Poulsen jana imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya DR Congo.

Mchezo huo ulikuwa wa kufuzu Kombe la Dunia dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa 1-1 na ni DR Congo walianza kumtungua Aishi Manula.

Bao la Tanzania lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 36 kwa shuti kali ambalo lilimshinda mlinda mlango wa DR Congo.

Pia katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe nyota wawili walionyeshwa kadi za njano ikiwa ni pamoja na Mzamiru Yassin na Feisal Salum hawa wote ni viungo wa kati.

Mchezo ujao wa Tanzania iliyo kundi J itacheza dhidi ya Madagascar unatarajiwa kuchezwa Septemba 7, Uwanja wa Mkapa.

Katika kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar Taifa Stars ipo kundi J ikiwa pamoja na DR Congo, Madagascar na Benin.