NA MWANDISHI WETU

TIMU ya Taifa ya Tanzinia (Taifa Stars) jana  ilifanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Madagascar.

Mchezo huo ni kuwania kufuzu Kombe la Dunia ulichezwa Uwanja wa Mkapa na hakukuwa na mashabiki kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Licha ya kushinda Madagascar walionyesha uwezo mkubwa na kucheza  kwa kujiamini, hivyo Stars ilipata wakati mgumu kushinda mchezo huo licha ya kuwa nyumbani.

Mabao ya Stars yalifungwa na Erasto Nyoni kwa mkwaju wa penalti Novatus Dismas na yote yalirudishwa kipindi cha kwanza na hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilikuwa sare ya mabao 2-2.

Kipindi cha pili baada ya mapumziko vijana wa Stars waliweza kujipanga na kusaka ushindi kwa juhudi.

Pasi ya upendo kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta ilikutana na miguu ya Feisal Salum ambaye alipachika bao la ushindi.