NA MADINA ISSA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la vyakula na rasilimali za baharini ‘Zanzibar Seafood Festival 2021’.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika hoteli ya Gold Zanzibar, iliyopo Kendwa mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja, alisema, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba 8 – 9, mwaka huu.

Alisema lengo la tamasha hilo ni kuunga mkono juhudi za utekelezaji wa sera za serikali chini ya uongozi wa Dk. Mwinyi katika kuendeleza sera ya uchumi wa buluu.

Alisema wananchi wa mkoa huo kwa muda mrefu wamekuwa wakiendesha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kupitia bahari na rasilimali zake na kutoa mchango mkubwa kwa taifa, hivyo serikali ya mkoa imeweka mkazo kuoanisha mchango huo ili uendane na hali za wananchi.

“Wananchi wetu wamekuwa wakiitumia bahari na kuuza mazao yake katika hoteli za kitalii lakini bado wamekuwa na hali duni, kupitia tamasha hili tutaweza kuwaunganisha moja kwa moja na mahoteli na wanunuzi wengine,” alieleza Ayoub.

Aliongeza kuwa hatua hiyo itachochea ukuaji wa uchumi na uwekezaji kupitia maliasili za bahari ikiwemo kuendeleza sekta ya utalii, uvuvi wa mazao ya baharini, biashara na usafirishaji.

Alifahamisha kuwa tamasha hilo, litahusisha makundi mbali mbali ya watu kutoka ndani na nje ya nchi ambao watakutana katika eneo la ufukwe wa kendwa kwa muda wa siku mbili.

Alieleza kuwa kupitia tamasha hilo, maeneo mbali mbali yatanufaika kupitia ujenzi wa miradi ya huduma za jamii ikiwemo ya madarasa, barabara na kuimarisha ujasiriamali.

“Wakaazi wa mkoa wa Kaskazini Unguja na maeneo mengine watapata fursa ya kuuza samaki na mazao ya baharini tani 150, kuwaunganisha kibiashara wavuvi wasiopungua 10,000 na wawekezaji wa hoteli za kitalii 127 zilizomo mkoani mwetu,” alieleza Ayoub.

Aliyataja manufaa mengine kuwa ni ajira za muda zisizopungua 16,322, ujenzi wa barabara ya lami kilomita 2.5, maonesho ya kazi za wavuvi na wajasiriamali