NA LAYLAT KHALFAN
CHAMA cha Wafanyakazi Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha huduma na Ushauri na zinazofanana na hizo (TUICO (Z)), kimetoa mkono wa pole kwa alie kuwa mwanachama wao, Aaliya Sened Riyami kilichotokea Augosti 23 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdi Omar Kombo, kwa niaba ya wanachama wa chama hicho, alifika nyumbani kwa marehemu Bububu Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, kwa lengo la kuifariji famiilia hiyo na kumtakia dua marehemu.
Alisema chama kimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa ya kuondokewa na mwanachama huyo, kwani ni mtu aliepigania haki nyingi za wafanyakazi.
Alisema Marehemu Aaliya, ni pengo lisilosahaulika milele hivi wataendelea kumkumbuka kwa mema aliyoyafanya katika kipindi chote cha uhai wake.
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Marehemu, Nassor Abdallullah Rashid, alisema walifurahi kupata ugeni huo kwa kwenda kuwafariji kwani ni ishara tosha ya kuwa ndugu yao alijali wafanyakazi wenzake.
Alikiomba chama hicho kuendelea kushirikiana na familia hiyo kwa kujenga uhusiano mwema na kumtaka Katibu huyo kama kuna mtu anamdai marehemu asisite kufika kwa ndugu wa marehemu kupata haki yake.
“Haimanishi kuwa ndugu yetu kafa ndio msije kufuata haki zenu hapa kwani kufanya hivyo ni kumweka marehemu mahala pazuri peponi”, alisema.