NA ASYA HASSAN

LICHA ya serikali na mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda kupigania haki za wanawake katika kupata fursa mbalimbali ili wajikwamue na hali duni ya maisha, bado baadhi ya wanawake wamekuwa wakijikosesha kupata fursa tofauti ikiwemo ajira katika baadhi ya makampuni binafsi.

Hali hiyo inatokana na kile kinachodaiwa kwamba ni tabia za baadhi ya wanawake hao kuwa chafu ikiwemo kutoridhika na hali zao za kimaisha na kusababisha kujiingiza katika makundi machafu ikiwemo wizi.

Hayo yamebainika kupitia kampuni ya Savannah International iliyopo Amaan Viwanda Vidogo Vidogo kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi wa kike na hatimae kuwafukuza mmoja badala ya mwengine kutokana na kipindi hicho kampuni hiyo kupata hasara kubwa kwa madai kwamba wafanyakazi hao walikuwa wakiiba nguo na kuitia hasara kubwa kampuni hiyo.

Ikiwa basi serikali na wadau tofauti kila uchao wakiendelea kutafuta njia na mikakati madhubuti ya kuwasaidia makundi hayo lakini upande mwengine kwa baadhi ya makampuni yanaonekana kukata tamaa ya kuwachukua wanawake hao kuwaajiri kutokana na tabia chafu za kinamama hao.

Serikali na wadau wamekuwa wakisisitiza wanawake hao kupewa nafasi za ajira kwa kuamini kwamba uwepo wao katika maeneo tofauti ni chachu ya kubadiliosha mazingira na kuonekana kwa sura mpya ya kuichumi.

Hilo linasemwa kwa sababu ya kuonekana wanawake waaminifu, wanajituma na wanajali sana maslahi ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Licha ya kuonekana hivyo mambo yamegeuka kwa kampuni ya Savannah International iliyopo Amaan Viwanda Vidogo Vidogo kwa kuwafukuza kazi wafanyaka wanawake waliyokuwa wakifanya kazi ndani ya kampuni hiyo.

Kampuni hiyo ambayo hapo zamani ilikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi wanawake kuliko wanaume lakini kutokana na tamaa zao na kutoridhika na kipato chao ndio kilichosababisha wafanyakazi hao kufukuzwa kazi mmoja badala ya mwengine.

Kampuni hiyo ililazimika kufanya hivyo kwa kile walichokidai kwamba kukithiri kwa wizi wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya kampuni hiyo.

Kampuni hiyo iliendelea kudai kwamba kutokana na hali hiyo ilisababisha kuwasimamisha kazi wafanyakazi hao mmoja badala ya mwengine kwani hawajui dhamira ya kufanya hivyo pengine ingeweza kusababisha kufilisika kwa kampuni hiyo.

Uwepo wa chombo hicho unasaidia asilimia kubwa ya watu kufanikisha maendeleo na harakati mbalimbali za maisha yao na hata serikali kutegemea kupata mapato yao kupitia eneo hilo hivyo endapo wangeifirisi na kuvunjika kwa biashara hiyo ingeweza kuleta athari kubwa.