BEIJING, CHINA

UBAGUZI wa rangi, mzozo wa mabadiliko ya tabianchi, janga la COVID-19 na mgawanyiko unaozidi kuongezeka duniani zitakuwa ajenda kuu zitakazojadiliwa kwenye Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa.

Rais wa China, Xi Jinping ameonya kuwa ulimwengu umeingia katika kipindi cha misukosuko mipya na mabadiliko.Rais wa Finland Sauli Niinisto, alisema wako katika wakati mgumu.

Naye Rais wa Costa Rica, Carlos Alvarado Quesada alisema ulimwengu wa baadae unapaza sauti kwao ikitaka kupunguzwa kwa matumizi ya silaha na kuwekeza zaidi kwenye amani.

Tathmini kali zaidi ya mzozo wa sasa duniani huenda ni ile iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwenye hotuba yake ya kuufungua mkutano huo, akiutaka ulimwengu kuamka.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan alisema janga la virusi vya corona linawakumbusha kwamba ulimwengu mzima ni sehemu ya familia kubwa.