NAIROBI, KENYA
UKUAJI wa uchumi Kenya umeshuka kwa kiwango cha asilimia 0.3 mwaka 2020 kutokana na athari za janga la virusi vya corona, licha ya uchumi huko kukua kwa asilimia tano mwaka 2019.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa na Waziri wa Fedha, Ukur Yattani, kiwango cha mfumuko wa bei kilipanda kutoka asilimia 5.3 mwaka 2019 hadi asilimia 5.4 mwaka 2020 kutokana na mikakati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, iliyodumaza usambazaji wa bidhaa.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 zinazoangazia mwaka 2020 kuhusu maendeleo ya uchumi Kenya, pato la taifa kutoka sekta ya utalii limepungua kwa asilimia 43.9 hadi shilingi bilioni 91.7 mwaka 2020 huku idadi ya wageni kwenye mahoteli ilipungua kwa asilimia 58.0 mwaka huo hadi watu milioni 3.8.
Idadi ya wageni waliowasili Kenya mwaka 2020 ilipungua kwa asilimia 71.5 hadi 579,600 ikilinganishwa na mwaka 2019.
Kiwango cha biashara kilipungua hadi shilingi trilioni 2.29 huku thamani cha bidhaa zilizoingizwa Kenya ikiwa ni shilingi trilioni 1.64 wakati thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi ikiwa ni shilingi trilioni 0.64.
Kwa usafiri wa ndege, idadi ya wasafiri ilipungua kwa asilimia 62.5 kutoka watu milioni 12.0 waliosafiri Kenya mwaka 2019 hadi watu milioni 4.5 mwaka 2020 wakati kiwango cha mizigo kikipungua kwa asilimia 8.9.
Kiwango cha mfumko wa bei za bidhaa kilipanda kutoka asilimia 5.3 mwaka 2019 hadi asilimia 5.4 mwaka 2020 kutokana na mikakati ya serikali ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, iliyolemaza usambazaji wa bidhaa na kuongeza bei za bidhaa hasa katika sekta ya uchukuzi na nishati, serikali inatarajia kiwango hicho kitaongezeka hadi mwishoni mwa mwaka 2021.
Wakati pato la mataifa yalio kusini mwa jangwa la Sahara likipungua kwa asilimia 1.9 mwaka 2020 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 3.2 mwaka 2019.
Serikali ya Kenya inaeleza kuwa sekta ya kilimo ilinawiri kwa asilimia 4.8 kutokana na uzalishaji na uuzaji wa kiasi cha juu wa chai, maharage, mchele na mtama na kiwango cha juu cha mvua kilichoshuhudiwa mwaka huo.
Charles Karisa, mshauri wa masuala ya uchumi nchini Kenya anaeleza kuwa Kenya haikuwekeza kwenye sekta muhimu kukinga uchumi wake.
Yattani, anaeleza kuwa sekta ya habari, mawasiliano na teknolojia ilinawiri kwa asilimia 4.8 kutokana na ongezeko la matumizi ya mifumo ya kiteknolojia ya kupokea na kutuma pesa kutumia simu na matumizi ya mifumo hiyo katika mafunzo wakati vituo vya mafunzo viliathirika kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Waziri Yattani, alieleza kuwa ajira katika sekta mbalimbali za uchumi ziliathiriwa vibaya na hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona lakini Kagame apandisha vyeo maafisa watano wa RDF kwa Kanali nyingi ya asilimia 83 ya ajira zilizopatikana mwaka 2020, zilitoka kwenye sekta ya biashara ndogo ndogo.