Youri Tielemans
KIUNGO wa Ubelgiji, Youri Tielemans, amesema, anaweka hatma yake wazi huku akiendelea kujadiliana kuhusu mkataba wake na klabu ya Leicester. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amehusishwa na uhamisho wa Liverpool, Manchester United , Barcelona na Real Madrid. (Sky Sports).

Harry Kane
MSHAMBULIAJI wa England, Harry Kaane huenda akatia saini mkataba mpya na Tottenham iwapo kifungu cha kumuachilia kuondoka katika kandarasi yake kitawekwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 awali aliamini kwamba alikuwa na makubaliano ya kiungwana na mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy kuondoka Spurs msimu huu wakati Manchester City ilipojaribu kumsaini. (Eurosport).

Lautaro Martinez
KLABU za Tottenham na Atletico Madrid ziliwasilisha ombi la dau la euro milioni 90 kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Lautaro Martinez ambalo lilikataliwa na klabu ya Inter Milan msimu huu huku Arsenal pia ikakataliwa baada ya kutoa ofa ya chini. (Gazzetta dello Sport).

Bukayo Saka
MSHAMBULIAJI wa Arsenal na England, Bukayo Saka amefuatiliwa na klabu tofauti, lakini, washika bunduki wanasema kwamba mchezaji huyo hashikiki. (Here We Go podcast).

Florian Wirtz
KIUNGO wa Bayer Leverkusen mwenye umri wa miaka 18, Florian Wirtz amevutia azma kutoka kwa baadhi ya klabu za Ligi Kuu ya England pamoja na Bayern Munich. (Express).

Jules Kounde
FURSA ya Chelsea ya kumsajili beki wa kati wa Sevilla mwenye umri wa miaka 22, Jules Kounde itategemea iwapo kandarasi ya beki wa Ujerumani Antonio Rudiger na mabingwa hao wa Ulaya itatatuliwa. (Star).

Georginio Wijnaldum
KIUNGO wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30), amesema, alitaka kusalia katika klabu ya Liverpool , lakini, akaondoka katika uhamisho wa bila ya malipo kuelekea PSG baada ya kuhisi kwamba ahitajiki na wekundu hao. (L’Equipe).

Houssem Aouar
ARSENAL haijafutilia mbali matumaini ya kumsajili kiungo wa Lyon na Ufaransa, Houssem Aouar na itamlenga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 msimu ujao.(Todofichajes).

Nahitan Nandez
KLABU ya Tottenham inatarajiwa kuwa miongoni mwa vigogo vitakavyomsajili kiungo wa Calgiari, Nahitan Nandez ambaye pia alikuwa akisakwa na Inter Milan, Napoli, Roma na Fiorentina wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari. Klabu hiyo ya ‘Serie A’ ipo tayari kumuuza mchezaji huyo mwaka mpya. (Tuttomercatoweb).

Axel Tuanzebe
KIUNGO wa zamani wa Manchester United na England, Axel Tuanzebe (23), anataka kuufanya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Aston Villa kuwa wa kudumu. (Sun).

Jude Bellingham
KLABU za Manchester City na Liverpool zinadaiwa kuwa azma ya kumsajili mchezaji wa England na Borussia Dortmund, Jude Bellingham (18) huku Wajerumani wakitaka euro milioni 100 ama zaidi ili kumruhusu kiungo huyo.(Bild).

Declan Rice
KLABU ya West Ham imemuwekea bei nyota wao, Declane Rice, si chini ya pauni milioni 100 kumuuza kiungo huyo.(football.london).

Mason Mount
CHELSEA inajiandaa kumpatia kandarasi mpya kiungo wa England, Mason Mount, hatua ambayo huenda ikamfanya mshahara wake kuongezeka hadi pauni 150,000 kwa wiki. (90min).

Alessandro Bastoni
KLABU ya Chelsea inaweza kuwanyatia mabeki wa Inter Milan na Italia, Alessandro Bastoni (22) na raia wa Slovakia Milan Skriniar. (Mediaset).