Serge Aurier
BEKI wa Ivory Coast, Serge Aurier (28), atakuwa huru kuhamia Arsenal baada ya kumaliza kandarasi yake huko Tottenham siku ya mwisho ya uhamisho. (Sky Sports).
Joules Kounde
BEKI wa Ufaransa, Jules Kounde (22), ana hasira na Sevilla kwa kutomuuza Chelsea. (Spanish Football Podcast).
Erling Braut Haaland
REAL Madrid iko tayari kumsaka mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland (21), na mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 22, Kylian Mbappe, msimu huu. (Marca).
Paul Pogba
MIAMBA hiyo ya Hispania pia wanavutiwa kumleta kiungo wa kati wa Ufaransa, Paul Pogba (28), Bernabeu kutoka Manchester United. (Marca).
Ole Gunnar Solskjaer
KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alizuia wachezaji watano kuondoka Old Trafford msimu huu. (Mirror).
Kyle Walker-Peters
KLABU ya Everton imemfuatilia mlinzi wa Muingereza wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, Kyle Walker-Peters katika siku za mwisho za usajili. (Telegraph).
Edinson Cavani
KLABU ya Juventus ilikataa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani (34), kutoka Manchester United muda mfupi baada ya mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 kuondoka klabuni hapo. (Mirror).
Adama Traore
KLABU ya Wolves inapanga kufuatilia tena hali ya mkataba wa winga, Adama Traore baada ya kukataa mkataba mara mbili kutoka Tottenham kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania. (Birmingham.Live).
Mariano Diaz
WAKALA wa Mariano Diaz, amesema kuna ‘kitu cha kushangaza kilichotokea’ kumzuia mshambuliaji huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 28 kujiunga na Valencia kutoka Real Madrid. (El Partidazo de Cope).
Djed Spence
KLABU za Leicester, Southampton na Nottingham Forest zote zilitoa ofa ya kuchelewa kwa beki wa kulia wa Middlesbrough, Djed Spence (21). (Northern Echo).
Emerson Royal
KOCHA wa Tottenham, Nuno Espirito Santo, alimhakikishia Emerson Royal (22), kwamba atakuwa na jukumu muhimu katika timu hiyo, kabla ya mlinzi huyo wa Brazil kukubali kuondoka Barcelona. (Marca).
Yves Bissouma
KLABU za Manchester United, Liverpool na Arsenal ziko tayari kupambana kumsaka kiungo wa Brighton na Mali, Yves Bissouma (25), mnamo mwezi Januari. (Mirror).
Malang Sarr
BEKI wa Chelsea raia wa Ufaransa, Malang Sarr (22), ameachwa kwenye njia panda baada ya mpango wake wa kuhamia timu ya Greuther Furth kwa mkopo kushindwa kufanikiwa siku ya mwisho ya uhamisho. (Mail).