ADAMA TRAORE

WOLVES wanataka kumfanya winga wa Uhispania Adama Traore, 25, mchezaji wao anayelipwa mshahara wa juu zaidi kwa mkataba mpya wa malipo ya pauni 120,000- kwa wiki kuzuia nia za klabu za Tottenham na Liverpool kumchukua. (Sun)

KYLIAN MBAPPE

REAL MADRID waliandaa mikataba saba ya kufanya mazungumzo na Kylian Mbappe huku wakiazimia kusaini mktataba na mshambuliajii huyo Mfaransa kabla ya muda wa mwisho wa kipindi cha uhamisho kutimia, lakini timu hiyo kubwa ya Uhispania ina matumaini makubwa kuwa Mbappe mwenye umri wa miaka 22, atajiunga nao kutoka Paris St-Germain mwaka 2022. (Sport – in Spanish)

EDUARDO CAMAVINGA

KIUNGO wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 18, aliishawishi Rennes kumuacha ajiunge na Real Madrid msimu huu licha ya kwamba PSG ilitoa ofa nzuri zaidi kwake binafsi na klabu yake ya zamani. (AS – in Spanish)

CRISTIANO RONALDO

PSG haikuwasilisha dau rasmi kwa ajili ya mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo licha ya kufanya mazungumzo juu ya uhamisho wa Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 kabla ya kuondoka Juventus kujiunga na Manchester United. (Le10Sport – in French)

PAULO DYBALA

JUVENTUS wanataka kujenga timu ndogo itakayomzingira Muagentina Paulo Dybala, 27, baada ya kukubali kumuacha Ronaldo arejee United. (Calciomercato – in Italian)

JESSE LINGARD

KIUNGO wa kati wa England Jesse Lingard, 28, alikataa fursa ya kujiunga na West Ham kwa mkataba wa kudumu kufuatia mkataba wa mkopo wa msimu uliopita katika Hammers ili kupigania nafasi yake katika Manchester United. (90Min)

BERND LENO

INTER MILAN ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mlindalango wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 37, ambaye anatarajiwa kuondoka the Gunners kwa uhamisho huru wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao . (Tuttosport – in Italian)

DANI OLMO

BARCELONA watajaribu kusaini mkataba na mshambuliaji Mhispania Dani Olmo, 23, kutoka klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig mwezi Januari, ambapo wamekubali kimsingi kumpatia mkataba wa miaka mitano. (Mundo Deportivo – in Spanish)

ANTOINE GRIEZMANN

BAADHI ya wachezaji wa kikosi cha Barcelona walionesha furaha yao baada ya kurejea kwa mshambuliaji Mfaransa Antoine Griezmann katika Atletico Madrid huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 akiripotiwa kuhangaika kupata nafasi yake katika Nou Camp. (Diario Sport – in Spanish)

TIEMOUE BAKAYOKO

KIUNGO wa kati Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 27, ana matumaini ya kuendelea kubaki katika klabu ya AC Milan baada ya mkataba wake wa mkopo kutoka Chelsea kumalizika. (Goal)

CARTER-VICKERS

MLINZI Mmarekani Cameron Carter-Vickers, 23, alipinga muda wa mwisho aliowekewa kwamba awe amehama kutoka Tottenham na kwenda Torino, kabla ya kupata mkataba wa mkopo katika Celtic. (Football Insider)

KYLE HUDLIN

CELTIC wanapanga kusaini mkataba na mchezaji mrefu sana , mwenye urefu wa futi 6 na inchi 9 , mshambuliaji Muingereza Kyle Hudlin, 21, ambaye anachezea klabu ya Ligi ya taifa hilo Solihull Moors. (Football Insider)

ROMEO

MTOTO wa kiume wa David Beckham Romeo, 19, amesaini mkataba na klabu ya Fort Lauderdale CF, inayocheza katika daraja la tatu katika Ligi ya soka ya Marekani . (Miami Total Futbol)