Ansu Fati
BARCELONA wanatarajia kumfunga Ansu Fati kwa nyongeza ya mkataba.
Fati anataka kubakia Camp Nou baada ya kuaminiwa na jezi namba 10 na klabu inapanga kumpa mkataba mrefu.(Mundo Deportivo).

Adama Traore
KLABU ya Wolves inataka kumfanya winga wa Hispania, Adama Traore (25), mchezaji wao anayelipwa mshahara wa juu zaidi kwa mkataba mpya wa malipo ya pauni 120,000- kwa wiki kuzuia nia za Tottenham na Liverpool kumchukua. (Sun).

Eduardo Camavinga
KIUNGO wa Ufaransa, Eduardo Camavinga (18), aliishawishi Rennes kumuacha ajiunge na Real Madrid msimu huu licha ya kwamba PSG ilitoa ofa nzuri zaidi kwake binafsi na klabu yake ya zamani. (AS).

Paulo Dybala
KLABU ya Juventus inataka kujenga timu ndogo itakayomzingira Muargentina, Paulo Dybala (27), baada ya kukubali kumuacha Cristiano Ronaldo arejee Manchester United. (Calciomercato).

Jesse Lingard
KIUNGO wa England, Jesse Lingard (28), alikataa fursa ya kujiunga na West Ham kwa mkataba wa kudumu kufuatia mkataba wa mkopo wa msimu uliopita kwa wangonga nyundo hao ili kupigania nafasi yake Manchester United. (90Min).

Bernd Leno
KLABU ya Inter Milan ni miongoni mwa vigogo vinavyomtaka mlinda mlango wa Arsenal na Ujerumani, Bernd Leno (37), ambaye anatarajiwa kuondoka kwa uhamisho huru wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao. (Tuttosport).

Dani Olmo
BARCELONA itajaribu kusaini mkataba na mshambuliaji Mhispania, Dani Olmo (23), kutoka RB Leipzig mwezi Januari, ambapo wamekubali kimsingi kumpatia mkataba wa miaka mitano. (Mundo Deportivo).

Tiemoue Bakayoko
KIUNGO wa Ufaransa, Tiemoue Bakayoko (27), ana matumaini ya kuendelea kubakia AC Milan baada ya mkataba wake wa mkopo kutoka Chelsea kumalizika. (Goal).

Cameron Carter-Vickers
MLINZI raia wa Marekani, Cameron Carter-Vickers (23), alipinga muda wa mwisho aliowekewa kwamba awe amehama kutoka Tottenham na kwenda Torino, kabla ya kupata mkataba wa mkopo katika Celtic. (Football Insider).

Hatem Ben Arfa
KIUNGO, Hatem Ben Arfa anaweza kujiandaa kujiunga na Rapid Bucharesti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa mchezaji huru tangu aondoke Bordeaux mwishoni mwa msimu uliopita na kituo chake chengine kinaweza kuwa Romania.(Pro Sport).