Theo Hernandez
MANCHESTER City na PSG wanamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto na nyuma wa AC Milan ana Ufaransa, Theo Hernandez (23). (Calciomercato).

Xherdan Shaqiri
HATUA ya Liverpool kushindwa kumuuza winga wa Uswizi, Xherdan Shaqiri (29), au mshambuliaji wa Ubelgiji, Divock Origi (26), imewafanya wakose nafasi ya kumsajili mshambuliaji Red Bull Salzburg raia wa Zambia, Patson Daka (22).(Express).

Jude Bellingham
KIUNGO wa England, Jude Bellingham (18), amedokeza huenda akajiunga na Liverpool huku meneja, Jurgen Klopp akijiandaa kuvamia klabu yake ya zamani ya Borussia Dortmund. (Star).

Paul Onuachu
LIVERPOOL pia wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Genk na Nigeria, Paul Onuachu (27) na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Mbelgiji huyo. (Mirror).

Karim Adeyemi
LIVERPOOL pia ni miongoni mwa klabu tatu ikiwemo Bayern Munich na Barcelona zinazopania kumsajili nyota kinda wa Red Bull Salzburg na Ujerumani, Karim Adeyemi (19), ambaye amefunga mabao sita katika mechi sita za Ligi Kuu msimu huu. (Bild).

Jules Kounde
CHELSEA wataendelea kumfuatilia beki wa Sevilla, Jules Kounde (22), kwa lengo la kumnunua mwezi Januari baada ya kumkosa msimu huu wa joto. (Evening Standard).

Wesley Ribeiro Silva
MANCHESTER City imemkosa Wesley Ribeiro Silva msimu huu baada ya dau lao la pauni milioni 6.5 la kumnunua winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 kukataliwa na Palmeiras. (Marca).

Mohamed Elneny
ARSENAL imekataa dau ililowasilishwa na klabu ya Uturuki ya Galatasaray kumnunua kiungo wa kati wa Misri, Mohamed Elneny (29). (Sky Sports).

Marco Asensio
KIUNGO wa kati wa Real Madrid, Marco Asensio (25), amekataa nafasi ya kujiunga na Tottenham au AC Milan msimu huu wa kiangazi, baada Mhispania huyo kudokeza kuwa hajatulia Real Madrid. (Marca).

Declan Rice
MANCHESTER United imepewa nafasi ya kumsaini kiungo wa West Ham na England, Declan Rice (22), msimu ujao baada ya Chelsea kuelekeza darubini yao kwa mchezaji mwengine. (Mirror).

Konstantinos Mavropanos
MLINZI wa Arsenal aliyesahaulika Mgiriki Konstantinos Mavropanos (23), huenda akapewa mkataba wa kudumu katika klabu ya Stuttgart ambayo sasa anaichezea kwa mkopo. (Bild).

Aaron Ramsey
KIUNGO wa Wales, Aaron Ramsey (30), amekataa ofa kadhaa za kuondoka Juventus wakati wa msimu wa kiangazi kwani anatarajia kuwa katika kikosi cha kwanza chini ya ukufunzi wa Massimiliano Allegri. (Calciomercato).