Robert Lewandowski
REAL Madrid watamsaka mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski (33), ikiwa watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Norway, Erling Braut Haaland (21), kutoka Borussia Dortmund msimu ujao. (AS).
Antonio Rudiger
KLABU ya PSG wanamtaka mlinzi wa Ujerumani wa miaka 28, Antonio Rudiger, ambaye mkataba wake na Chelsea umesalia na chini ya mwaka mmoja kumalizika. (Le10Sport).
Declan Rice
MANNCHESTER United wamemtambua mchezaji wa kimataifa wa England na West Ham, Declan Rice (22), kama chaguo lao la kwanza dirisha la uhamisho litakapofunguliwa majira ijayo ya kiangazi. (Manchester Evening News).
Fabio Carvalho
REAL Madrid na klabu kadhaa za England zinamfuatilia kwa karibu mchezaji wa Fulham, Fabio Carvalho (19). Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Ureno, ana chini ya mwaka mmoja katika mkataba wake kabla ya kuondoka uwanja wa Craven Cottage. (Mail).
Jude Bellingham
KLABU ya Borussia Dortmund wamekubaliana juu ya mkataba mpya na kiungo wa England, Jude Bellingham (18), na hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo msimu ujao licha ya kwamba ananyatiwa na klabu kadhaa za Ligi ya Primia. (90Min).
Lionel Messi
LIONEL Messi (34), amesisitiza kuwa mkataba wake na klabu ya Paris St-Germain inajumuisha kifungu ambacho kitamuwezesha kuipatia kipaumbele kiwakilisha Argentina kimataifa badala ya kuichezea klabu hiyo kuelekea michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujayo nchini Qatar. (Sport ).
Philippe Coutinho
BARCLONA italazimika kuilipa Liverpool kiasi cha euro milioni 20 kama marupurupu ya ziada ikiwa mchezaji, Philippe Coutinho (29), ataiwakilisha zaidi ya mara 100 klabu hiyo ya La Liga. Mchezaji huyo amecheza mechi 90 za Barca tangu alipojiunga nao.(Goal).
Nampalys Mendy
UHAMISHO wa mkopo wa kiungo wa Leicester, Nampalys Mendy (29), kwenda Galatasaray umegonga mwamba kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal hawezi kufika Istanbul kabla ya dirisha la uhamisho la Uturuki kufungwa. (Foot Mercato).
Franck Kessie
KIUNGO, Franck Kessie huenda akaondoka AC Milan mwezi Januari mwakani baada ya kiungo huyo wa Ivory Coast aliye na miaka 24, kukataa ofa ya mkataba wa thamani ya euro milioni 6.5 kwa mwaka kutoka kwa klabu hiyo ya Serie A. (Tuttosport).
Thiago Alcantara
LIVERPOOL ni miongoni mwa klabu zinazomtaka Kessie, ijapokuwa Milan huenda ikatafuta mkataba wa kubadilishana wachezaji, ikizingatiwa kwamba kiungo wa kati wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Hispania, Thiago Alcantara (30), anahamia San Siro. (Il Milanista).
David Luiz
MLINZI wa zamani wa Arsenal, David Luiz (34), anapania kurejea nyumbani kwao Brazil baada ya kupuuza ombi la Marseille. (Le10Sport).
Mesut Ozil
NYOTA mwengine wa zamani wa Arsenal, Mesut Ozil (32), ananyatiwa na klabu kadhaa za MLS na Qatar baada ya mkataba wa kiungo huyo wa Ujerumani kumalizika Fenerbahce. (AS).