Matthias Ginter
KLABU ya Tottenham ina azma ya kumsajili beki wa kati wa Borussia Monchengladbach, Matthias Ginter, lakini, inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich na Real Madrid ili kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Ujerumani. (Calciomercato).

Axel Tuanzebe
KIUNGO wa zamani wa Manchester United na England, Axel Tuanzebe (23), anataka kuufanya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Aston Villa kuwa wa kudumu. (Sun).

Paul Pogba
KIUNGO wa Ufaransa, Paul Pogba (28), ambaye amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na PSG na Real Madrid, anelekea kuongeza kandarasi yake Manchester United baada ya Cristiano Ronaldo kurudi Old Trafford. (Athletic).

Jude Bellingham
KLABU za Manchester City na Liverpool zinadaiwa kuwa azma ya kumsajili mchezaji wa England na Borussia Dortmund, Jude Bellingham (18) huku Wajerumani wakitaka euro milioni 100 ama zaidi ili kumruhusu kiungo huyo.(Bild).

Declan Rice
KLABU ya West Ham imemuwekea bei nyota wao, Declane Rice, si chini ya pauni milioni 100 kumuuza kiungo huyo.(football.london).

Mason Mount
CHELSEA inajiandaa kumpatia kandarasi mpya kiungo wa England, Mason Mount, hatua ambayo huenda ikamfanya mshahara wake kuongezeka hadi pauni 150,000 kwa wiki. (90min).

Timo Werner
KLABU ya Bayern Munich inataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na Chelsea, Timo Werner (25), Januari. (Football Insider).

Jesse Lingard
KLABU ya Leicester City ina azma ya kumsajili kiungo wa Manchester United na England, Jesse Lingard. (Fichajes).

Alessandro Bastoni
KLABU ya Chelsea inaweza kuwanyatia mabeki wa Inter Milan na Italia, Alessandro Bastoni (22) na raia wa Slovakia Milan Skriniar. (Mediaset).

Franck Kessie
KLABU ya Tottenham imewasilisha ofa ya kumsajili kiungo wa AC Milan, Franck Kessie (24), ijapokuwa haijulikani iwapo Spurs itawasilisha ombi hilo au kusubiri kumsaini mchezaji huyo wa Ivory Coast katika uhamisho wa bila ya malipo mwezi Januari (Calciomercato).

Callum Hudson-Odo
MENEJA wa Chelsea, Thomas Tuchel, amesema, walifanya uamuzi wa busara kutomuachilia winga wa England, Callum Hudson-Odoi (20), kuondoka siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji. (Football London).

Karim Adeyemi
CHELSEA wamefanya mazungumzo ya kumsajili kinda matata wa Ujerumani, Karim Adeyemi (19), miaka mitatu iliyopita hawajafanikiwa kumpata mshambuliaji huyo wa Red Bull Salzburg. (Sunday Express).

Alexandre Lacazette
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Alexandre Lacazette (30), anaweza kuondoka baada ya klabu kujaribu kumsaka, Tamy Abraham (23) kuwa mbadala wake, kabla ya kuondoka Chelsea kuelekea Roma. (Mirror).

Ansu Fati
WINGA wa Barcelona na Hispania, Ansu Fati amepewa ofa na klabu kadhaa za juu za Ulaya, ikiwemo Manchester City.(El Nacional).