RAHEEM STERLING

BARCELONA ina mpango wa kujaribu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa England na Manchester City Raheem Sterling, 26, mwezi Januari baada ya kushindwa kumleta Nou Camp majira ya joto. (Sport – in Spanish)

MINO RAIOLA

WAKALA wa Paul Pogba Mino Raiola anasema kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28-huenda akajiunga tena na Juventus wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Rai Sport via Corriere dello Sport – in Italian)

GONZALO HIGUAIN

MSHAMBULIAJI wa Inter Miami Gonzalo Higuain anasema klabu hiyo ya MLS ina ndoto ya kumsajili Lionel Messi wakati mkataba wa nyota huyo na Paris St-Germain itakapomalizika mwaka 2023. (ESPN Argentina – in Spanish)

NABY KEITA

LIVERPOOL wameanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita,26. Kandarasi yake ya sasa inamalizika mwaka 2023. (Calciomercato – in Italian)

KAYKY

MSHAMBULIAJI Kayky, 18, raia wa Brazil ameanza kufanya mazoezi na Manchester City baada ya klabu hiyo kusongeza mbele uhamisho wake kutoka Fluminense, ambao awali ulikuwa ukamilishwe Januari. (Manchester Evening News)

ANTONIO RUDIGER

TOTTENHAM huenda wamefufua upya mpango wao wa kumsaka beki wa Ujerumani Antonio Rudiger mkataba wake na Chelsea usiporefushwa msimu ujao. (Express)

THOMAS TUCHEL

MKUFUNZI wa Chelsea Thomas Tuchel anasema kuna “sababu nyingi ” ya Rudiger kuondoka lakini beki huyo wa kati hajatilia maanani uvumi unaoendelea. (Mail)

ALEXANDRE LACAZETTE

MENEJA wa Arsenal Mikel Arteta anasema mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30- Alexandre Lacazette, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao, atakuwa kiungo ”muhimu”kwa kikosi chake msimu huu . (Metro)

GEORGINIO WIJNALDUM

KIUNGO wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, “amechoka” na uhamisho wake kwenda Paris St-Germain kutoka Liverpool ulikuwa “makosa”, kulingana na mwandani wake wa karibu. (L’Equipe – in French)

SERGI ROBERTO

MLINZI wa Uhispania Sergi Roberto, 29, atasaini kandarasi mpya na Barcelona wiki chache zijazo baada ya kufikia mkataba na rais wa klabu hiyo Joan Laporta. (Marca)

CALLUM HUDSON-ODOI

WINGA wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 20, anafiria kubadili uaminifu wake wa kimataifa kutoka England na kwenda Ghana. (Mail)

SEAN DYCHE

KOCHA wa Burnley Sean Dyche ana matumaini wachezaji kadhaa watasalia katika klabu hiyo kufuatia hatua yake ya kusaini kandarasi. (Times – subscription required)

DECLAN RICE

MANCHESTER UNITED wamemuorodhesha mchezaji wa West Ham Declan Rice kuwa kipaumbele chao majira ya joto. Kiungo huyo wa kati wa England aliye na umri wa miaka 26 alikuwa tayari kuhamia Old Trafford na alisikitika sana kwamba bei ya Hammers ya pauni milioni 100 ilimkosesha nafasi ya kuondoka dirisha la uhamisho lilipofunguliwa. (Independent)