Alexandre Lacazette
MSHAMBULIAJI wa Arsenal na Ufaransa, Alexandre Lacazette (30), hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu. (Le10 Sport).
Matthijs de Ligt
CHELSEA wanataka kumsajili beki wa kati wa Juventus na Uholanzi, Matthijs de Ligt (22). (Mirror).
Loris Karius
FC Basel inafikiria kumchukua mlinda lango wa Liverpool na Ujerumani, Loris Karius (28). (Bild).
Roberto Martinez
BARCELONA italazimika kulipa euro milioni 1.8 ili kumtoa Roberto Martinez kutoka kwa mkataba wake na timu ya taifa ya Ubelgiji. (Sport).
Ronald Koeman
LAKINI, Martinez, amepuuza ripoti zinazomuhusisha na kazi hiyo kama mbadala anayeweza kuchukua nafasi ya Mholanzi aliye chini ya shinikizo, Ronald Koeman (58). (Eurosport).
Antonio Rudiger
KLABU ya Bayern Munich ina nia ya kumsajili beki wa Chelsea na Ujerumani, Antonio Rudiger, lakini, mchezaji huyo wa miaka 28 anataka kusaini mkataba mpya huko Stamford Bridge. (Bild).
Marco Asensio
KLABU ya Liverpool wanamtazama winga wa Real Madrid na Hispania, Marco Asensio (25) (Fichajes).
Thomas Tuchel
KOCHA wa Chelsea, Thomas Tuchel amedokeza kwamba kiungo wa England, Ruben Loftus-Cheek (25), anapaswa kumvutia ili kuokoa maisha yake ya ‘Blues’. (Express).
Liam Delap
MANCHESTER City wamekataa dau la pauni milioni 15 kutoka Borussia Dortmund kwa mshambuliaji wa Uingereza, Liam Delap (18) (Football Insider).
Noa Lang
KLABU ya Arsenal na AC Milan wana nia ya kumsajili winga wa Uholanzi wa Club Brugge, Noa Lang (22). (Express).
Carl Rushworth
SKAUTI wa Barcelona wamemtazama mlinda mlango wa Brighton, Carl Rushworth (20), ambaye kwa sasa yuko mkopo huko Walsall. (Mirror).
Matthias Ginter
KLABU ya Tottenham ina azma ya kumsajili beki wa kati wa Borussia Monchengladbach, Matthias Ginter, lakini, inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich na Real Madrid ili kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Ujerumani. (Calciomercato).
Axel Tuanzebe
KIUNGO wa zamani wa Manchester United na England, Axel Tuanzebe (23), anataka kuufanya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Aston Villa kuwa wa kudumu. (Sun).
Jude Bellingham
KLABU za Manchester City na Liverpool zinadaiwa kuwa azma ya kumsajili mchezaji wa England na Borussia Dortmund, Jude Bellingham (18) huku Wajerumani wakitaka euro milioni 100 ama zaidi ili kumruhusu kiungo huyo.(Bild).