Federico Chiesa
KLABU ya Borussia Dortmund inaweza kuwasilisha ombi la kumsajili winga wa Juventus na Italia, Federico Chiesa (23), endapo klabu hiyo ya Bundesliga itampoteza mshambuliaji wa Norway, Erling Braut Haaland (21), msimu ujao wa joto. (Calciomercato).

Tanguy Ndombele
KLABU ya Tottenham inaweza kuwa tayari kumuachilia kiungo wa Ufaransa, Tanguy Ndombele (24), katika makubaliano ya kubadilishana na raia mwenzake mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial. (Express).

Jarrod Bowen
LIVERPOOL bado inaweza kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Uingereza wa West Ham, Jarrod Bowen. Walihusishwa na ofa ya pauni milioni 20 kwenye dirisha la majira ya joto. (Liverpool Echo).

Marco Asensio
KIUNGO wa Real Madrid, Marco Asensio (25), pia ni miongoni mwa wanaolengwa na Liverpool. (Fichajes.Net).

Paulo Fonseca
MENEJA wa Ureno, Paulo Fonseca (48), anasema hatua yake ya kuisimamia Tottenham ilitibuka kwa sababu mkurugenzi wa michezo, Fabio Paratici alitaka Spurs icheze mpira wa ‘safu ya kujilinda’.(Telegraph).

Antonio Rudiger
BEKI wa Chelsea na Ujerumani, Antonio Rudiger (28), hatokimbilia uamuzi juu ya maisha yake ya baadaye, lakini, anataka nyongeza ya mshahara ikiwa atabakia Stamford Bridge. (90min).

Julian Nagelsmann
MENEJA wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, amesema, bado hajazungumza na Mkurugenzi wa Michezo, Hasan Salihamidzic, kuhusu Rudiger, ambaye atakuwa hana mkataba mpya mwaka ujao. (Eurosport).

Alexandre Lacazette
KLABU ya Arsenal inatarajiwa kumpoteza mshambuliaji wa Ufaransa, Alexandre Lacazette bure wakati mkataba wake utamalizika msimu wa joto, na Atletico Madrid inavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Le10 Sport).

Ousmane Dembele
MANCHESTER United wamefanya mawasiliano na Barcelona juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa, Ousmane Dembele (24). (El Nacional).

Matthijs de Ligt
CHELSEA wanataka kumsajili beki wa kati wa Juventus na Uholanzi, Matthijs de Ligt (22). (Mirror).

Loris Karius
FC Basel inafikiria kumchukua mlinda lango wa Liverpool na Ujerumani, Loris Karius (28). (Bild).

Roberto Martinez
BARCELONA italazimika kulipa euro milioni 1.8 ili kumtoa Roberto Martinez kutoka kwa mkataba wake na timu ya taifa ya Ubelgiji. (Sport).

Ronald Koeman
LAKINI, Martinez, amepuuza ripoti zinazomuhusisha na kazi hiyo kama mbadala anayeweza kuchukua nafasi ya Mholanzi aliye chini ya shinikizo, Ronald Koeman (58). (Eurosport).