Nordi Mukiele
MANCHESTER United inamuangalia, Nordi Mukiele kama beki mpya wa kulia.
Beki huyo wa RB Leipzig anaonekana kama mrithi wa Aaron Wan-Bissaka, na ‘mashetani wekundu’ wakikusudia kutumia nyota yao iliyopo kama sehemu ndogo kwenda mbele.
(Fichajes).
Agustin Alvarez
ATLETICO Madrid ndiyo klabu ya karibuni kujiunga na mbio za kumsaka, Agustin Alvarez, na mshambuliaji huyo wa Penarol ameingiwa kwenye rada zao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Uruguay aliyeichezea mara mbili, yuko kwenye rada ya vigogo kadhaa vya Ulaya pamoja na mabingwa hao wa La Liga. (Goal).
Caglar Soyuncu
KIUNGO, Caglar Soyuncu yuko kwenye rada ya Real Madrid wakati Los Blancos inataka kuimarisha ulinzi wao.
Beki huyo wa kati wa Uturuki, anayevutia akiwa na Leicester City, yuko kwenye orodha ya matamanio huko Santiago Bernabeu. (Goal).
Isco
AC Milan wamefanya mazungumzo kadhaa na Real Madrid juu ya kumsaini Isco na wanazidi kujiamini kutua kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye ameanza mara mbili tu msimu huu, alikuwa huru kuondoka Los Blancos wakati wa kiangazi, lakini, hakufikia makubaliano na watu wowote wanaopenda.(Todofichajes).
Luis Diaz
KLABU ya Barcelona imemtaja mshambuliaji wa Porto, Luis Diaz kama mchezaji atakayesajiliwa msimu ujao wa joto.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia, ambaye amelinganishwa na mwenzake James Rodriguez, amefunga mabao matano katika michezo sita ya ligi akiwa na Porto msimu huu.
(El Nacional).
Oscar Garcia
KOCHA wa Reims, Oscar Garcia ndiye mgombea wa hivi karibuni kumrithi, Ronald Koeman huko Barcelona.
Koeman yuko chini ya shinikizo baada ya kuanza vibaya msimu na bodi ya Barca inaaminika kujadili nafasi zinazoweza kubadilishwa. (RMC Sport).
Reece James
CHELSEA itataka wachezaji wanne kutoka Real Madrid kama mpango wa kumruhusu mlinzi wa kulia, Muingereza Reece James (21). (Express).
Marquinhos
KLABU ya Chelsea itaachana pia na mpango wake wa kumuwania mlinzi wa Ufaransa kutoka Sevilla, Jules Kounde (22), na mlinzi wa kati wa PSG, Mbrazil Marquinhos (27), ili kuelekeza nguvu zake za kumsajili mlinzi wa Juventus na Uholanzi mwenye umri wa miaka 22, Matthijs de Ligt. (Star).
Philippe Coutinho
BARCELONA watamuuza kiungo wake mchezeshaji raia wa Brazil, Philippe Coutinho (29), katika dirisha la usajili la Januari. (Marca).
Bukayo Saka
KLABU ya Atletico Madrid inamtaka mshambuliaji wa Arsenal na England mwenye umri wa miaka 22, Bukayo Saka. (La Razon).