Youssef En-Nesyri
ARSENAL itamtoa mshambuliaji wa Ufaransa, Alexandre Lacazette (30), kwa Sevilla kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Morocco mwenye umri wa miaka 25, Youssef En-Nesyri. (La Razon).
Kalvin Phillips
LEEDS United imeanza mazungumzo ya mkataba na kiungo wa England, Kalvin Phillips kwa nia ya kutompoteza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa wapinzani wao Manchester United. (Star).
Sam Johnstone
KLABU ya Tottenham inamtaka kipa wa West Brom na England, Sam Johnstone (28). (Football Insider).
Harry Winks
SPURS pia imesema ipo tayari kumuachilia kiungo wa England, Harry Winks (25), kuondoka mwezi Januari wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. (Caughtoffside).
Declain Rice
KIUNGO wa England, Declan Rice, amesema anaridhika kuwa West Ham na anaweza kufikia malengo yake katika klabu hiyo. Rice mwenye umri wa miaka 22 anahusishwa na tetezi za kujiunga na Chelsea na Manchester United. (Sky Sports).
Florian Wirtz
MANCHESTER City wanamnyatia kiungo wa Bayern Leverkusen mwenye umri wa miaka 18 Mjerumani, Florian Wirtz. (Bild).
Pau Torres
CHELSEA inafikiria kumleta mlinzi wa Villarreal, Pau Torres (24), katika klabu hiyo. Manchester United pia wanamtaka Mhispania huyo. (90min).
Bernd Leno
INTER Milan hawataki kumsaini kipa wa Arsenal na Ujerumani, Bernd Leno (29). Klabu hiyo ya ‘Serie A’ badala yake inamsaka mchezaji wa kimataifa wa Cameroun wa Ajax, Andre Onana (25). (Fabrizio Romano).
Jules Kounde
KIUNGO wa Ufaransa, Jules Kounde, amesema atazingatia Sevilla baada ya dau la Chelsea kushindwa kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wakati wa kiangazi. (Star).
Dusan Vlahovic
RAIS wa Fiorentina, Rocco Commisso amesema klabu hiyo inajizatiti kumshawishi, Dusan Vlahovic ambaye pia ananyatiwa na Arsenal na Chelsea kusaini mkataba mpya. Mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka, 21, alifunga magoli 21 ya ‘Serie A’ msimu uliopita. (Express).
Gonzalo Villar
KLABU ya Everton inamfuatilia kiungo wa Roma, Gonzalo Villar (23), baada ya kubaini kuwa mchezaji huyo hayupo katika mipango ya kocha, Jose Mourinho ya klabu hiyo. (Fichajes).
Pedro Porro
REAL Madrid inafikiria kupeleka ofa kwa ajili ya mlinzi wa pembeni wa Hispania, Pedro Porro (22), ambaye yuko kwa mkopo Sporting Lisbon akitokea Manchester City. (O Jogo).
Franck Kessie
KLABU za Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa vigogo vya England vinavyotajwa kumfuatilia kiungo wa Ivory Coast, Franck Kessie (24), ambaye amegoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya AC Milan. (90min).
Tom Davies
CRYSTAL Palace wanamfuatilia kwa makini, Tom Davies (23) wa Everton kufuatia hali ya sintofahamu ya mustakabali wa kiungo huyo wa Kiingereza. (Football Insider).
Nordi Mukiele
MANCHESTER United inamuangalia, Nordi Mukiele kama beki mpya wa kulia.
Beki huyo wa RB Leipzig anaonekana kama mrithi wa Aaron Wan-Bissaka, na ‘mashetani wekundu’ wakikusudia kutumia nyota yao iliyopo kama sehemu ndogo kwenda mbele.
(Fichajes).
Agustin Alvarez
ATLETICO Madrid ndiyo klabu ya karibuni kujiunga na mbio za kumsaka, Agustin Alvarez, na mshambuliaji huyo wa Penarol ameingiwa kwenye rada zao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Uruguay aliyeichezea mara mbili, yuko kwenye rada ya vigogo kadhaa vya Ulaya pamoja na mabingwa hao wa La Liga. (Goal).
Caglar Soyuncu
KIUNGO, Caglar Soyuncu yuko kwenye rada ya Real Madrid wakati Los Blancos inataka kuimarisha ulinzi wao.
Beki huyo wa kati wa Uturuki, anayevutia akiwa na Leicester City, yuko kwenye orodha ya matamanio huko Santiago Bernabeu. (Goal).
Luis Diaz
KLABU ya Barcelona imemtaja mshambuliaji wa Porto, Luis Diaz kama mchezaji atakayesajiliwa msimu ujao wa joto.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia, ambaye amelinganishwa na mwenzake James Rodriguez, amefunga mabao matano katika michezo sita ya ligi akiwa na Porto msimu huu.
(El Nacional).