Franck Kessie
MANCHESTER United wamemtaja kiungo wa AC Milan na Ivory Coast, Franck Kessie (24), kama mbadala wa nyota wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28, Paul Pogba ambaye mkataba wake Old Trafford unamalizika mwaka 2022. (Mundo Deportivo).

Tanguy Ndombele
MCHEZAJI mwenzake Pogba katika timu ya taifa Tanguy Ndombele ni kiungo mwengine kwenye rada ya Manchester United aliyehamia Tottenham kwa pauni milioni 53.8 mnamo 2019. (Calciomercato).

Andreas Christensen
BEKI wa Denmark, Andreas Christensen yuko tayari kusaini nyongeza ya mkataba huko Chelsea wenye thamani ya pauni 120,000 kwa wiki baada ya awali kupewa ofa ya mshahara wa chini kuliko pauni 78,000. (Sun).

Bukayo Saka
JUVENTUS na Atletico Madrid ni miongoni mwa klabu zinazomwangalia winga wa Arsenal na England, Bukayo Saka (20). (Calciomercato).

Marquinhos
REAL Madrid inapanga kumsajili beki wa Paris St-Germain, Marquinhos (27), huku Mbrazil huyo akiwa chini ya mkataba katika klabu hiyo ya Ufaransa hadi 2024. (Fichajes).

Noa Lang
LEEDS United bado wanavutiwa na winga wa Uholanzi wa Club Bruges, Noa Lang (22). (Football Insider).

Dusan Vlahovic
KLABU ya Fiorentina wanajaribu kumfunga mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic kwa mkataba mpya baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuhusishwa na kuhamia Tottenham msimu ujao wa joto.(Gazzetta dello Sport).

Danny Drinkwater
KIUNGO wa England, Danny Drinkwater, anakiri maisha yake ya Chelsea yamekuwa ‘katika hali mbaya’ baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuanza kucheza Reading katika uhamisho wa mkopo wake wa nne mbali na Stamford Bridge. (talkSPORT).

Alexis Sanchez
KLABU ya Inter Milan ina azma ya kumuachilia mshambuliaji wa Chile, Alexis Sanchez huku Real Betis na Sevilla zikionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (InterLive).

Kingsley Coman
MIAMBA mitatu inajipanga kumsajili, Kingsley Coman kutoka Bayern Munich.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa anatafutwa na Liverpool, Tottenham na Juventus na anaweza kuwa kwenye harakati kwenye dirisha lijalo la uhamisho.(Fichajes).

Charles De Ketelaere
AC Milan wana nia ya kumsaini, Charles De Ketelaere kutoka Club Brugge.
Rossoneri anataka nambari mpya 10 na wanamuona kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 kama chaguo bora kufuatia maonyesho yake ya kupendeza.(Goal).

Raheem Sterling
BARCELONA wanaangalia uhamisho wa mkopo kwa winga wa Manchester City, Raheem Sterling.
Sterling amekosa upendo wa ManCity katika kipindi hiki na inasemekana yuko wazi kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani, Sergio Aguero huko Camp Nou. (Sport).

Gonzalo Higuain
MSHAMBULIAJI wa Inter Miami, Gonzalo Higuain, amesema, klabu hiyo ya MLS ina ndoto ya kumsajili Lionel Messi wakati mkataba wa nyota huyo na Paris St-Germain itakapomalizika mwaka 2023. (ESPN Argentina).

Naby Keita
KLABU ya Liverpool imeanzisha mazungumzo ya kandarasi mpya na kiungo wa Guinea, Naby Keita (26). Kandarasi yake ya sasa inamalizika mwaka 2023.
Aidha, mshambuliaji, Kayky (18), raia wa Brazil ameanza kufanya mazoezi na Manchester City baada ya klabu hiyo kusogeza mbele uhamisho wake kutoka Fluminense, ambao awali ulikuwa ukamilishwe Januari. (Manchester Evening News).