NA ALI KINASA SUZA (SCCM)

MSEMAJI   Mkuu  wa  Hospitali  ya Rufaa ya Mnazimmoja, Dokta  Hassan  Makame Mcha, amesema Hosptali hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba  wa wafanyakazi jambo ambao linasababisha utolewaji wa huduma kuwa duni.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wanodai hawapati huduma kwa wakati hasa wanapopokelewa na wanafunzi wanaosema kada hiyo.

Mmoja ya wananchi hao aliiambia Zanzibar Leo, Sikuzani Juma, alisema  mara  nyingi  suala  hilo  hufanywa  na  baadhi ya  madaktari  waliopo  katika  mafunzo ya vitendo hali inayowapa masaibu wagonjwa.

Amesema  ni jambo la kawaida kwa madaktari hao kufanya dharau kwani hupokea wagonjwa na kuwaweka  katika  vitanda  vya  hospital   bila  ya kuwapatia  huduma.

Akijibu tuhuma hizo, msemaji huyo alisema suala hilo halina ukweli kwa  wagonjwa  wanaofuata  huduma  za matibabu hospitalini  hapo na changamoto iliyopo hospitalini hapo ni uhaba wa wafanyakazi jambo linalopelekea baadhi ya wakati kuchelewa kutolewa kwa huduma.

“Ikitokea mfanyakazi kuchelewa kufanya kazi kwa wakati basi hua ana kazi zaidi ya moja na hii inatokana na uhaba wa wafanyakazi, madktari ni kidogo kuliko idadi ya wagonjwa, kwa hiyo ni vyema kuongezwa wafanyakazi ili kuongeza ufanisi kwenye utendaji hospitalini hapa” alibai