KABUL, AFGHANISTAN

UMOJA wa Mataifa utafanya kongamano la kuchangisha fedha  mjini Geneva kwa juhudi zake za kuchangisha zaidi ya dola milioni 600 kwa ajili ya  Afghanistan.

Umoja huo unaonya kwamba huenda kukawa na mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo kufuatia Taliban kuchukua madaraka.

Kongamano hilo litahudhuriwa na maofisa wakuu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Katibu Mkuu Antonio Guterres na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas.

Hata kabla Taliban kuuteka mji wa Kabul mwezi uliopita, nusu ya idadi ya watu nchini Afghanistan au watu milioni 18 walikuwa wanategemea misaada.

Umoja wa Mataifa unatahadharisha kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na ukame na uhaba wa fedha na chakula.

Mataifa mengi ya kigeni yalisitisha utupaji wa misaada ya kifedha kwa Afghanistan kufuatia Taliban kuchukua madaraka jambo lililouwekea shinikizo kubwa Umoja wa Mataifa.