WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibar Leo Jumapili, leo katika safu hii ya maakuli lnimewatayarishia upishi mwanana wa vitumbua vya kuku.
Jaribu leo hii na uone namna upishi huu ulivyo mtamu kwani wengi wamezuea kupika vitumbua vya nyama yam ng’ombe.
Hivyo wikiendi hii ni bora kubadilisha na kupika vitumbua hivi na utaona mabadiliko yake kwa namna familia itakavyopenda upishi huu.
Basi fuatilia namna ya mahitaji yanayotakiwa, vipimo na namna ya kupika vitumbua vya nyama ya kuku.
VIPIMO
Kuku – 3 Lb
Mayai – 6
Baking Powder – 1 kijiko cha chai
Pilipili boga – Robo kipande
Kitunguu maji – 1 kidogo
Pilipili manga ya unga – 1 kijiko cha chai
Kitunguu saumu(thomu) na Tangawizi – 1 kijiko cha supu
Chumvi – ½ kijiko cha chai
Mafuta ya kuchomea
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Chemsha kuku mpaka awive. hakikisha umemchemsha na viungo vyote. baada ya kuwiva, toa mifupa kwa kunyambua mnofu vipande vidogo vidogo.
- Kata kitunguu vipande vidogo vidogo
- Kata pilipili boga (la kijani) vipande vidogo
- Tia vitu vyote hivyo katika mashine la kusagia (Blender)
- Tia mayai, hakikisha mayai yanafunika mchanganyiko.
- Saga kwa muda mfupi tu.
- Weka mchanganyiko uliosagika vizuri kwenye bakuli.
- Tia chumvi, pilipili manga na baking powder.
- Tayarisha chuma cha kuchomea vitumbua kwenye jiko.
- Weka mafuta kidogo.
- Choma kama unavyochoma vitumbua vya mchele.