TRIPOLI, LIBYA

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za watoto la  limetahadharisha kuwa, utoaji elimu kwa watoto katika robo ya nchi za dunia ambazo zimeathirika na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi, maambukizi ya COVID-19 na zisiso na mawasiliano ya kidijitali unakabiliwa na changamoto kubwa.

Shirika hilo limetangaza kuwa, mfumo wa utoaji mafunzo kwa watoto huko Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia, Afghanistan, Sudan Kusini, Mali na Libya unakabiliwa na hatari kubwa, na kwamba nchi za Syria na Yemen zinafuata mkondo huo.

Shirika hilo lisiso la kiserikali limechapisha ripoti na kuashiria takwimu zinazoonyesha kuwa,asilimia 90 ya wanafunzi duniani hawaendi skuli wakati huu wa maambukizi ya COVID-19.

Shirika hilo la kimataifa limetahadharisha kuwa, janga la corona ni moja tu kati ya vitisho vingi vilivyoutumbukiza hatarini mfumo wa kutoa elimu kwa watoto duniani.

Limesema, mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi na mazingira kama vimbunga, mafuriko au ukame ni sababu nyengine ambazo kila mwaka hupelekea karibu nusu ya watoto milioni 75 waliotimiza umri wa kwenda skuli kulazimika kukatiza masomo yao.