MEXICO, MEXICO

MAHAKAMA ya juu zaidi ya Mexico imetoa uamuzi kwamba adhabu dhidi ya utoaji mimba ni kinyume cha katiba.

Uamuzi huo ambao ni ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa kutetea afya na haki za wanawake, umejiri wakati baadhi ya majimbo ya Marekani yalitangaza sheria kali dhidi ya utoaji mimba.

Hukumu hiyo inamaanisha kuwa Mahakama katika taifa hilo haziwezi kuruhusu au kuendesha kesi dhidi ya utoaji mimba.

Hukumu hiyo inafuata uamuzi wa kihistoria uliotolewa Argentina mapema mwaka huu uliohalalisha utoaji mimba.

Rais wa mahakama hiyo ya Mexico Arturo Zaldivar aliusifu uamuzi huo akisema ni mabadiliko ya kihistoria kwa wanawake hasa walioko katika hatari.

Mexico iliyo na takriban waumini milioni 100 wa kanisa Katoliki ndilo taifa kubwa zaidi la kikatoliki katika kanda hiyo baada ya Brazil.Kanisa Katoliki linapinga utoaji mimba.