ZASPOTI
BONDIA, Oscar Valdez, amekana kwamba alikuwa ametumia dawa zilizopigwa marufuku hapo awali, na ana mpango wa kufuata masharti ya tume kusonga mbele na pambano lake la Septemba 10 dhidi ya Robson Conceicao, litakalopigwa Casino Del Sol huko Tucson, Arizona.

Promota wa bingwa huyo wa uzito wa manyoya wa WBC, alitangaza kwenye ‘twitter’ kwamba pambano lake na Conceicao, litafanyika kama ilivyopangwa mnamo Septemba 10.

Ingawa, Valdez, anakanusha kutumia dawa iliyopigwa marufuku, alipima na kukutwa na ‘phentermine’ kwenye moja ya vipimo, dawa ya kupunguza uzito.
Mapema juzi, Baraza la Ndondi Ulimwenguni lilisema kwamba Valdez anaweza kupigana na Conceicao. Kwa kuongezea, Tume ya Wanamichezo ya Pascua Yaqui pia iliamua kuwa Valdez ni vizuri kuendelea na pambano lake.

“Vipi kuhusu watu wangu, nataka kuwambia kwamba sijawahi kutumia dawa zilizokatazwa kuimarisha kiwango, sijawahi kufanya hivyo na sitofanya hivyo”, alisema, Valdez.(AFP).