HAFSA GOLO NA MUZNAT HAJI (SCCM)

SERIKALI imesema kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa vifaa vya michezo kwa watu wenye ulemavu, huwafanya kushindwa kushiriki michezo ya kitaifa na kimataifa.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita alieleza hayo ukumbi wa baraza la Wawakilishi, wakati akijibu suala lililoulizwa na mwakilishi nafasi za wanawake Mwantatu Mbarak Khamis, alipotaka kufahamu mpango wa serikali wa kuwapatia vifaa watu wenye ulemavu ili washiriki mashindano mbali mbali.

Alisema pamoja na changamoto hiyo wizara hiyo, imeandaa orodha ya mahitaji ya vifaa kwa michezo yote hapa Zanzibar ikiwemo ya watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuwasilisha kwa wahisani mbali mbali wa ndani na nje.

Aliongeza kwamba hatua hiyo ni kuona watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa kama watu wengine katika ushiriki wa masuala ya michezo nchini.

“Vyama vya michezo ya watu wenye ulemavu nao wameomba kuwasilisha aina ya vifaa wanavyohitaji mazingatio”, alisema.