JAKARTA, INDONESIA

WAFUNGWA  41 wamekufa katika ajali ya moto uliotokea kwenye gereza moja lililokuwa na idadi kubwa ya wafungwa katika jimbo la Banten nchini Indonesia.

Moto huo ulizuka wakati wafungwa wengi walipokuwa wamelala.Walinzi walijaribu kufungua milango lakini ilishindikana kutokana na moto kuwa mkubwa.

Kwa jumla walikuwepo wafungwa 122 kwenye sehemu iliyopaswa kuwa na wafungwa 40.

Mfungwa mmoja miongoni mwa waliokufa alitoka Afrika Kusini.Baada ya kwenda kwenye sehemu ya ajali, waziri wa sheria na haki za binadamu wa Indonesia Yasonna Laoly alisema watu wapatao 80 walijeruhiwa katika ajali hiyo ya moto.