NA ZAINAB ATUPAE

WANAMICHEZO 75 kutoka nchi mbali mbali duniani wameshiriki mashindano ya ‘Ceo Golf Day’, yaliofanyika hoteli ya Sea Cliff Mangapwani.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kumalizika mashindano hayo meneja wa mashindano Elias Soka, alisema lengo la mashindano ni kukuza na  utalii wa Zanzibar pamoja na  kuutangaza mchezo huo kitafa na kimataifa.

Alisema malengo mengine ni kuuendeleza  na kuhamasisha utalii wa Zanzibar kwa kuamini kuwa ni nchi muhimu yenye utulivu.

Akizitaja nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni pamoja na Kenya,Tanzania,Uganda,Rwanda, AfikaKusini, Sweden, Ujerumani, Marekani, Canada, Uingereza ,Malawi, Ubelgiji na Sudan.

Mussa Fumu ni mchezaji  kutoka Zanzibar,aliomba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuurejesha uwanja wa Gofu uliokuwepo Maisara ili mchezo huo kuwa kivutio kikubwa cha watalii wanaokuja Zanzibar.

Alisema mchezo huo unaweza kuleta mafanikio makubwa kwani watalii wengi wanapokuja hupenda kucheza,lakini wanakosa sehemu ya wazi ya kuchezea.

“Uwanja upo kinachotakiwa ni kufanyiwa marekebisho,ili mchezo huo uendelee kwani watalii wanakuja wengi kwa ajili ya kuicheza,”alisema.