ABUJA, NIGERIA

WANAFUNZI 73 wametekwa nyara na watu wenye silaha katika skuli ya sekondari ya kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Kulingana na taarifa rasmi ya polisi, Kundi la watu wenye silaha lilivamia skuli hiyo ya eneo la Kaya katika mkoa wa Maradun la Jimbo la Zamfara na kuwateka nyara wanafunzi hao.

Timu za uokozi za polisi zinafanya kazi pamoja na wanajeshi kujaribu kuwakomboa wanafunzi hao, alisema msemaji wa polisi Mohammed Shehu.

Utekaji nyara wa wanafunzi umekuwa ni jambo lilozoeleka kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria.Karibu wanafunzi 1,000 walitekwa mwaka huu na baadae wengi wao waliachiliwa.

Rais Muhammadu Buhari yuko chini ya shinikizo kutokana na nchi yake kukosa usalama.Licha ya juhudi za wanjeshi za kupambana na wahalifu hao, mashambulizi na utekaji nyara bado yanaendelea.