KHARTOUM, SUDAN

VIONGOZI wa kijeshi nchini Sudan wamesema viongozi wa kisiasa nchini humo walio katika mgawanyo wa madaraka, ndio waliofungua mlango wa jaribio la mapinduzi kwa kuweka kando maslahi ya umma na kuingia katika ugomvi binafsi.

Katika kile ambacho kinaonekana kama ukosoaji usio wa kawaida,wakizungumza katika mahafali ya kijeshi ya Omdurman, Mkuu wa Baraza Kuu la Kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, Mohamed Hamdan Dagalo walisema viongozi hao wamesahau msingi wa mapinduzi dhidi ya Omar al Bashir ya 2019.

Tangu kufanyika mapinduzi hayo, mpango wa kugawanya madaraka kati ya jeshi na raia umekuwa ukiyumba.

Mamlaka ya kijeshi ilisema inawashikilia maofisa 21, ambao walitaka kufanya jaribio la mapinduzi mapema siku hiyo.