MOSCOW, URUSI

WATU watano wamekufa wakipanda Mlima Elbrus, mlima mkubwa kabisa nchini Urusi na Ulaya, shirika la habari la TASS liliripoti Ijumaa.

Waokoaji waliwashusha watu wengine 14 kutoka mlima TASS wakinukuu afisa kutoka Wizara ya Dharura ya Urusi. Watu hao walipatiwa matibabu.

Kikundi cha wapanda mlima kiliomba msaada wakati walipofika umbali wa urefu wa mita 5,400 siku ya Alhamisi kutokana na hali mbaya ya hewa.