HAVANA, CUBA
CUBA imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuanza kuwapa watoto walio na umri wa kuanzia miaka miwili chanjo dhidi ya COVID-19 kwa kutumia chanjo waliyojitengenezea lakini ambayo imetambuliwa na Shirika la Afya Duniani WHO.
Taifa hilo la kisiwa lenye jumla ya watu milioni 11.2 linatarajia kuwachanja watoto wote kabla ya skuli ambazo zimefungwa tangu mwezi Machi mwaka uliopita kufunguliwa.
Ijumaa iliyopita Cuba alianza kampeni yake ya chanjo kwa watoto kwa kuwachanja wale wenye umri wa miaka 12 na zaidi.
Nchi hiyo ilianza kutoa chanjo kwa watoto wenye kati ya umri wa miaka miwili na 11.
Nchi kama China, Umoja wa Falme za Kiarabu na Venezuela zimetangaza mpango wa kuwapa watoto wachanga chanjo.