KINSHASA, CONGO
TAKRIBAN watu 30 wameuawa katika shambulio kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Vyanzo vya ndani na vya UN vilisema wanajihadi wa kikosi cha (ADF) wanashukiwa kufanya shambulio hilo katika eneo la Ituri.
Dieudonne Malangayi, kaimu mwenyekiti wa ufalme wa Walese Vonkutu, mwanzoni alisema watu 14 walifariki katika shambulio hilo .
Raia waliokwenda kutafuta miili ya waathirika walipata wengine 16 msituni, jambo ambalo linawafanya raia 30 kuuawa.Raia mmoja ambaye alisaidia kutafuta miili alisema waathirika walishambuliwa zaidi kwa mapanga na risasi.
ADF, ambayo Marekani imeliona kuwa kundi la kigaidi, inachukuliwa kuwa baya zaidi ya wanamgambo wenye silaha ambao huzunguka mashariki mwa Kongo DR.