WASHINGTON,MAREKANI

WATU kote kaskazini mashariki mwa Marekani bado wanafanya usafi, zaidi ya siku moja baada ya dhoruba kulikumba eneo hilo.

Watu wasiopunua 39 waliuawa huku zaidi ya makaazi 150,000 yakikosa umeme.

Dhoruba hiyo ndio iliyobakia kutokana na kimbunga Ida.Mvua ya rikodi ya sentimita 18 ilinyesha zaidi ya saa 24 katika eneo la Central Park jijini New York.

Mvua hiyo ilisababisha mafuriko yaliyoingia kwenye makaazi ya watu.

Baadhi ya watu walizama kwenye majengo yaliyo chini ya ardhi,Mafuriko hayo yalinasa watu katika magari yao.Maji yalifurika katika vituo vya treni vya chini ya ardhi. Na yalilazimisha mamlaka za uwanja wa ndege kufuta mamia ya safari za ndege.

Dhoruba hiyo ilisababisha kimbunga huko New Jersey. Upepo uliezua paa za nyumba na kubomoa nyumba kwenye mtaa mmoja.

Rais Joe Biden alikiri kwamba matukio ya hali mbaya ya hewa sasa ni suala la kawaida.Aliahidi kuwa serikali kuu itasaidia kupeleka chakula, maji, na mahitaji mengine.