NEW DELHI, INDIA

WATU watatu pamoja na jambazi wameuawa siku ya Ijumaa katika majibizano ya risasi ndani ya chumba cha korti katika mji mkuu wa India Delhi, polisi walisema.

Ufyatuaji huo wa risasi ulifanyika katika maeneo ya uwanja wa mahakama ya Rohini kaskazini mwa Delhi.

Kulingana na polisi, wanaume wawili walikuwa wamevaa mavazi kama ya mawakili waliofyatuliwa risasi na jambazi Jitender Gogi ndani ya chumba cha mahakama, na kumuua papo hapo. Hata hivyo washambuliaji walipigwa risasi mara moja na wafanyakazi wa usalama wakiwa kazini.

Polisi walisema kushambuliwa kwa Gogi kulitokana na vita vya genge haramu.

Gogi alihusika katika visa kadhaa vya jinai na kufungwa huko Tihar alikuwa akifikishwa mahakamani wakati washiriki wa genge hilo hasimu walipomshambulia.

“Watu wawili kutoka genge pinzani walimpiga risasi Jitender Gogi ndani ya mahakama huku polisi waliokuwepo hapo walilipiza kisasi haraka na kuwaua washambuliaji hao wawili,” afisa mwandamizi wa polisi alisema. “Jumla ya watu watatu wamekufa, pamoja na Gogi.”

Tukio la kufyatua risasi lilisababisha hofu ndani ya uwanja wa mahakama.

Kwenye picha zilizorushwa kwenye vituo vya habari vya televisheni milio ya risasi iliweza kusikika na polisi na mawakili walionekana wakitembea kwa hofu.

Ripoti zilisema kuwa kiwanja cha mahakama ya Rohini ni eneo lenye usalama mkubwa na wageni hukaguliwa vizuri kabla ya kuingia kwenye eneo hilo. Walakini, tukio la kufyatua risasi linaonyesha upungufu mkubwa wa usalama ndani ya jengo hilo.