DAMASCUS, SYRIA

ZAIDI ya watu 350,209 wameuawa nchini Syria katika muongo mmoja uliopita, taarifa hiyo ni kwa mujinbu wa Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa kati ya Machi 2011 hadi Machi 2021 watu 350,209 wamebainika kuwa wameuawa katika mapigano nchini Syria.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet aliyotoa katika kikao cha 48 cha Baraza la Haki za Binadamu la umoja humo, ambapo alisema: idadi hiyo inajumuisha watu walioweza kutambulika majina yao kamili, tarehe waliyofariki na mkoa waliofia.

Bi Bachelet alibainisha kwamba, taarifa zozote zisizojumuisha mambo hayo matatu zimefutwa; na uhakiki mpana umefanywa ili kuepusha kukusanywa taarifa za kukaririwa.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa alifafanua kuwa, katika watu hao 350,209 waliotambuliwa kuwa wameuawa katika mapigano hayo, kati ya kila watu 13, mmoja miongoni mwao ni mwanamke na mmoja ni mtoto.

Aliongeza kuwa hakuna shaka kwamba idadi ya watu waliouawa katika mapigano nchini Syria ni kubwa zaidi ya hiyo lakini idadi hiyo ndiyo ya watu walioweza kutambuliwa.

Tangu mwaka 2011, Syria inashuhudia vita dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo vilivyoanzishwa na makundi ya kigaidi ya wapiganaji kutoka nchi zaidi ya 100 duniani yanayoungwa mkono na madola ya eneo na nje ya eneo, lengo likiwa ni kuiangusha serikali hiyo…/