TUNIS,TUNISIA

MAELFU ya wananchi wa Tunisia wamemiminika katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa nchi hiyo Tunisia kulalamikia hatua ya karibuni ya Rais wa nchi hiyo Kais Saeid ya kumfukuza kazi Waziri Mkuu na kulifunga bunge.

Wananchi wa Tunisia walifanya maandamano na huku wakitaka kusambaratishwa mapinduzi, wanataka katiba ya nchi, uhuru  pamoja na kufunguliwa bunge la nchi hiyo haraka iwezekanavyo.

Maandamano hayo yalishuhudiwa pia katika miji mbalimbali ya Tunisia.

Wanasiasa na wanaharakati wa Tunisia awali walitaka kufanyika maandamano makubwa katika miji mbalimbali nchini humo.

Rais Kais Saeid wa Tunisia Julai 26 mwaka huu alimfukuza kazi Hicham Mechichi aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kusitisha shughuli za bunge.

Rais wa Tunisia katika hatua yake hiyo aliwaondolea pia wabunge kinga ya kisheria na kujipa mamlaka ya uendeshaji nchi hadi pale itapoundwa serikali mpya nchini humo.

Hatua hiyo ya Rais wa Tunisia ilitawaja na wapinzani wake kuwa sawa na mapinduzi dhidi ya serikali.