NA AHMED MAHMOUD ARUSHA

Msichana wa Kizanzibari Asma Ally 23 Mkazi wa Unguja ameibuka mshindi wa shindano la kuandika andiko la mradi kwa kujipatia hundi ya Milioni 12.5 baada ya kupata mafunzo ya B/U/S yaliondeshwa na taasisi za TRIAS, TAHA na AHA.

Shindano hilo la ujasiriamali limekuja mara baada ya kuwakutanisha wakulima na wafugaji waliopatiwa mafunzo kwa zaidi ya watu 500, walionufaika kutoka Arusha na Zanzibar, na hatimaye kupatikana watu 20  waliongia hatua hiyo baada ya mchujo.

Akiongea mara baada ya kupata fedha hizo, Asma alisema fedha hizo zitamsaidia kununua dawa za kuendeleza shughuli zake za ufugaji na ukulima wa tungule, pilipili hoho na mazao mengine ya mboga mboga kwa kuanzia na heka moja kwenye heka nane alizonazo.

Alisema kuwa anazishukuru Taasisi hizo kwa kuja na mafunzo hayo yaliomsaidia kuwa wa mwanzo kwenye shindano hilo la ujasiriamali na kuwataka kuendeleza mafunzo hayo, kwa lengo la kusaidia ndoto za wakulima kulima kisasa na kupata maendeleo chanya kiuchumi.

Kwa Upande wake Mohamed Ally Juma mkazi wa Chakechake amejizolea kiasi cha Milioni 7.5 kwenye shindano hilo huku alieleza kuwa shindano hilo limekuwa ni muendelezo wake kumsaidia siku za mbeleni awezekuwa kilelezo cha wakulima

Alisema fedha hizo ambazo watapata vifaa vitamsaidia kununua solar pump, ambayo itapunguza matumizi ya mafuta ambayo yamekuwa yakizalisha gesi ukaa, hivyo kuongeza tija katika kilimo na kuokoa uharibifu wa mazingira.

Awali akiongea mara baada ya kukabidhi zawadi, Angelina Nyansambo Afisa ufikiaji wa mitaji na maendeleo ya biashara,  alisema kuwa lengo lao ni kuona kilimo cha mboga mboga kinamnufaisha mkulima na wao kama TAHA amejipanga kuwasaidia wakulima hao kulima kisasa nakufikia malengo yao.

Alisema ipo haja kwa wakulima wanachama wa TAHA waliopata mafunzo ya B/U/S kujiona wamesogea kwenye malengo ya maendeleo yenye chachu ya kuongeza jitihada za kukuwa kiuchumi.

Mafunzo hayo yaliolenga kuwapatia mafunzo wakulima na wafugaji zaidi ya 500 yameendeshwa kwa ufadhili wa Taifa la Ujerumani na Taasisi ya TRIAS kwa kuendeshwa na TAHA.

Teknolojia ya kilimo asili cha biashara imeelezwa kuwa ndio mkombozi wa kuinua uchumi na kuokoa mazingira kutokana na utumiaji wa mbolea asili katika kukuza mimea na kuongeza mazao.

Kwa muktadha huo TAHA imetoa mafunzo na kuja na shindano lililokuwa na lengo la kusaidia wanachama wake wakishirikiana na Taifa la Ujerumani na Taasisi ya TRIAS kiweza kuandaa Andiko la mradi kuinua masoko na uboreshaji wa kilimo cha mbogamboga.