LONDON, UINGEREZA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson yupo katika jitihada ya kurekebisha mahusino ya taifa lake na Ufaransa baada ya kufanyika biashara ya pamoja ya nyambizi ya nyuklia kati ya Marekani, Uingereza na Australia.

Pamoja na kwamba hatua hiyo iliigadhibisha Ufaransa, lakini Johnson akiwa njiani kuelekea New York, Marekani alinukuliwa na vyombo vya habari akisema Uingereza inajivunia mahusiano yake ya Ufaransa.

Rikodi zinaonesha Uingereza na Ufaransa zinashirikiana katika operesheni za pamoja nchini Mali na kwenye mataifa ya Baltiki lakini pia katika programu kadhaa za pamoja za majiribio ya kinyuklia.